UONGOZI WA YOUNG AFRICANS SC WAKABIDHI VIFAA NA MAHITAJI KWA HOSPITALI YA RUFAA TEMEKE – MWANAHARAKATI MZALENDO

Uongozi wa Klabu ya Young Africans SC kwa kushirikiana na GSM Foundation, SportPesa, na Benki ya CRDB umekabidhi vifaa na mahitaji mbalimbali kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke. Tukio hilo lilifanyika leo katika hospitali hiyo ambapo vifaa vilikabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Hospitali, Dr. Joseph Kimaro.

Hii ni sehemu ya jitihada za klabu hiyo katika kurejesha kwa jamii kuelekea Kilele cha Wiki ya Mwananchi Jumapili hii. Young Africans SC imekuwa na utaratibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii kila mwaka wakati wa Wiki ya Mwananchi, kama njia ya kurudisha shukrani kwa jamii inayoendelea kuiunga mkono klabu hiyo. Tukio la Jumapili linatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi pamoja na wadau mbalimbali wa michezo.

#KonceptTvUpdates

Related Posts