WATAALAM WA MAABARA MUHIMBILI ( UPANGA&MLOGANZILA) WADHAMIRIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

 

  

Wataalam wa Maabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila ) wamekutana kwa lengo la kujadili na kutathimini utendaji kazi wa maabara ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma na kuhakikisha maabara za Muhimbili zinaendelea kukidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema mkutano huo umefanyika kwa siku mbili ili kuangalia na kufanya tathimini ya maabara za hospitali hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

“Wataalam wetu wamekuja na maazimio maalum hivyo wao na sisi menejimenti tutashirikiana kwa pamoja ili kuyatekeleza maazimio hayo kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi “ ameeleza Dkt. Magandi

Amefafanua kuwa mkutano huo pia ni matakwa katika mchakato wa kupata cheti cha ithibati ya ubora kimataifa katika maabara za hospitali hiyo ambapo kwa upande wa MNH Upanga jumla ya vipimo 58 tayari vimepata ithibati ya kimataifa na kwa upande wa MNH Mloganzila vipimo 44 navyo vimepata ithibati ya kimataifa .

“Tunaendelea kufanya maboresho mbalimbali na matarajio yetu katika tathimini inayokuja tataongeza vipimo zaidi ambavyo vitapata ithibati ya ubora kimataifa”amesisitiza Dkt Magandi

Related Posts