WATUMISHI WA AFYA 1,100 WANUFAIKA NA MKAPA FOUNDATION – MWANAHARAKATI MZALENDO

Taasisi ya Mkapa Foundation kwa miaka 18 sasa imetoa nuru kwa watumishi wa afya na taifa kwa ujumla, kwa kuwasaidia watu mbalimbali wenye uhitaji kwa kuwasomesha zaidi ya watu 1000 nchini.

Hayo yameelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipohudhuria hafla ya kukmbukizi ya tatu ya urithi wa aliyekuwa rais wa awamu ya tatu hayati Benjamin Mkapa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Dat es salaam leo.

“Serikali inaridhika sana na inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hii ya Benjamin Mkapa Foundation, ndani ya miaka 18 taasisi imesomesha watumishi wa afya watarajiwa na watumishi walioko kazini takribani 1,100 katika fani mbalimbali zikiwemo za matibabu, wauguzi wakunga n.k.” alisema Rais Samia Suluhu.

Aidha, aliongeza kuwa, “Urithi aliotuachia Hayati Rais Benjamin Mkapa, unamfanya aendelee kuishi hata baada ya kifo chake. Mzee Mkapa anakumbukwa kama Baba wa taasisi, Baba wa mifumo na Baba wa mageuzi. Mioyo yetu imeendelea kuwa na kumbukumbu ya urithi wa maarifa na urathi yaani ‘legacy’, urathi wake katika mifumo ya uongozi wa nchi yetu, tunaendelea kuishi nayo hadi sasa.”

 

#KonceptTvUpdates

 

Related Posts