Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na waratibu wa miradi inayotekelezwa na wizara yake makao makuu ya wizara eneo la Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 31 Julai 2024.
Waratibu aliokutana nao ni wale wanaotekeleza Miradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini (LTIP), Mradi wa Uwekeji Miundombinu ya Upimaji (LDI) pamoja na mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK)
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe, Ndejembi amesema uamuzi wa kukutana na waratibu wa miradi kwanza ni kupata ufahamu wa miradi inayotekelezwa na wizara kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati za Bunge mapema mwezi Agosti 2024.
Mhe. Ndejembi aliteuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivi karibuni akichukua nafasi ya Mhe. Jerry Silaa aliyehamishiwa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.