MKURUGENZI wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited, David Mulokozi amesema Watanzania wapenda burudani ya muziki sasa watakuwa na nafasi ya kuwashuhudia wasanii wakongwe wa muziki katika jukwaa moja baada kuingia nao mkataba wa kutangaza bidhaa za kampuni hiyo.
David Mulokozi amewataja wasanii hao kuwa ni Juma Nature, Matonya, Ferouz, Daz Baba, Domokaya na wengine wambao watapata fursa ya kukutana kwenye majukwaa kutoa burudani katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mbeya, Dodoma na Iringa.
“Nimefurahi sana kuona wasanii wetu wakiongozwa na Juma Nature,Matonya, Ferouz, Daz Baba, Domokaya na wengine wengi nina hakika mkataba huu utakua na manufaa kwa pande zote mbili Bongo Recods na kampuni yetu ya Mati Super Brands Limited,” amesema Mulokozi.
Katika upande mwingine Mkurugenzi wa Bongo Records ambaye ni ‘producer’ mkongwe Pfunk Majani amesema kuwa wamejipanga kufanya matamasha makubwa ndani na nje ya nchi.
“Tumejipanga kurudisha heshima ya Bongo Fleva tunaishukuru sana Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kutoa udhamini huu unaowawezesha wasanii kuwa mabalozi wa vinywaji wanavyozalisha,” alisema Pfunk.
Aidha wakongwe hao akiwemo Juma Nature, Jay Mo na Linah wameishukuru kampuni hiyo kwa kuingia mkataba huo unaowawezesha kufanya makubwa kwenye tasnia hiyo na kuahidi kufanya makubwa.
Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi Mati Super Brands Limited imesaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja na Kampuni ya Muziki ya Bongo Records inayoongozwa na ‘Producer’ PFunk Majani kwa lengo la kuwezesha matamasha mbalimbali ya muziki. Kampuni hiyo inazalisha vinywaji vya Tanzanite Royal Gin, Strong Dry Gin,Tanzanite Premium Vodka