WAKATI Ligi ya Mpira wa kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikiendelea Uwanja wa Donbosco Oysterbay, imeonyesha timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo zimeanza kujigawa katika makundi matatu.
Makundi hayo ni ya timu zinazowania kucheza hatua ya nane bora, zinazopambana kubaki kwenye ligi na zinazojinusuru zisishuke daraja.
Timu tisa zinawania kucheza hatua ya nane bora ambazo ni Dar City yenye pointi 40, UDSM Outsiders (38), Savio (36), JKT (32), Mchenga Star (31), Vijana ‘City Bulls’ (31) ABC (28) Srelio (28) na DB Oratory (27) na moja itashuka na kubaki nane.
Upande wa zinazopambana kusalia kucheza ligi ya BDL mwakani ni Ukonga Kings pointi 26, KIUT (25) na Pazi (25).
Zile zinazopambana zisishuke daraja ni Crows (23), Mgulani JKT (22), Jogoo, (22) na Chui (19) na tatu zinatakiwa kushuka.