MAJERAHA MAZITO YAIKUMBA UNITED – MWANAHARAKATI MZALENDO

Manchester United yaingia kwenye changamoto baada ya beki wao mpya, Leny Yoro, aliyenunuliwa kwa Pauni milioni 59 (takriban Tsh. bilioni 204), kupata jeraha litakalomuweka nje kwa miezi mitatu. Pamoja na hiyo, straika Rasmus Hojlund pia atalazimika kuwa nje kwa wiki sita kutokana na jeraha alilopata.

Majeraha haya yalitokea katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal uliofanyika Julai 27, 2024, ambapo Yoro aliumia mguu wa kushoto na Hojlund alipatwa na jeraha la nyama za paja.

Katika hali hii, kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, atakuwa na kazi ngumu ya kumtumia Joshua Zirkzee katika nafasi ya Hojlund. Kwa upande wa beki wa kati, Lisandro Martinez bado hajarejea kutoka katika majukumu yake ya Copa America, hivyo kwa sasa, ten Hag anategemea Harry Maguire, Jonny Evans, na Victor Lindelof kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi wa timu.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts