MATREKTA 10,000 KUWAFIKIA WAKULIMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Katika kuadhimisha sherehe za Nane Nane mwaka huu, Waziri wa Kilimo Mh. Hussein M Bashe katika ukurasa wake wa X amesema, “serikali ya Awamu ya 6 imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo. Kati ya hatua kubwa zitakazochukuliwa ni pamoja na kununua matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030, ambayo yatasaidia kuboresha shughuli za kilimo nchini”.

Aidha aliongeza kuwa, matukio muhimu katika maadhimisho haya ni pamoja na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutazamia na kuongoza sherehe za Nane Nane, Uwekaji jiwe la msingi kwenye maboresho ya Uwanja wa Agriculture Master Plan, Uzinduzi wa Mwongozo wa Zana za Kilimo na vituo vya zana mpya na Kuanzishwa kwa Mwongozo wa Shamba Darasa la Kilimo Biashara.

Kwa kuzingatia Agenda 10/30, hatua hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya kilimo na kuboresha maisha ya wakulima nchini.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts