Mamia ya waandamanaji vijana wamemiminika katika miji kadhaa ya taifa hilo, kupinga mageuzi ya serikali wanayodai kwamba yamezidisha hali ya maisha kuwa mbaya zaidi. Mamlaka za nchi hiyo zimesambaza maafisa wa usalama katika juhudi za kukabiliana na aina yoyote ya ghasia. Katika jiji la kibiashara la Lagos, waandamanaji walikusanyika kuelekea majengo ya serikali yaliyokuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kabla ya kuelekea maeneo mawili ambayo yamepangwa kufanyika maandamano hayo.
Na huko kaskazini katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kano, waandamanaji walijaribu kuwasha moto nje ya ofisi ya gavana na polisi waliwajibu kwa kuwarushia mabomu ya kutoa machozina kuwarudisha nyuma waandamanaji wengi. Takriban watu 1,000 waliandamana kwa amani katika eneo la bara la mji mkuu wa kiuchumi wa Lagos, na kuimba “Tinubu Ole”, neno la Kiyoruba linalomaanisha mwizi. Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mamia ya waandamanaji pia wamejitokeza katika mji wa kaskazini-mashariki wa Maiduguri, jimbo la Bauchi, na majimbo mengine kadhaa nchini kote.Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya
Barabara zilikuwa zimefungwa katika sehemu fulani za nchi na baadhi ya waandamanaji waliobeba mabango au vikosi vya usalama vilivyojihami, vilivyosambazwa usiku kucha baada ya siku kadhaa za uhamasishaji wa maandamano dhidi ya serikali ya Rais Bola Tinubu. Baadhi ya makundi pia yalifanya maandamano ya kumuunga mkono kiongozi huyo wa Nigeria.Nigeria yajiandaa kwa maandamano kupinga gharama ya maisha
Biashara nyingi nazo pia zilifungwa huku kukiwa na hofu kwamba maandamano hayo yanaweza kugeuka kuwa ya vurugu kama ya mwaka 2020 ya kupinga ukatili wa polisi katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Mmoja wa vijana aliyejitokeza amesema kwamba hawatorudi nyuma katika mapambano yao.
“Hatutaacha hadi pale kila Mnigeria atakapoweza kuishi kwa raha nchini Nigeria. Hatutaacha hadi pale sisi Wanigeria tunaoishi ndani, tutafurahia maisha sawa au maisha bora kuliko hata nchi nyingine ulimwenguni ambazo hazina nusu ya rasilimali tulizo nazo.”Kwanini Afrika inazongwa na maandamano ya vijana?
Maandamano hayo yanafanyika chini ya Hashtag ya komesha utawala mbovu Nigeria, ikiwa ni vuguvugu lililopata uungwaji mkono kupitia mitandao ya kijamii. Taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika linakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa thamani ya Naira baada ya Rais Bola Tinubu kuondoa ruzuku ya mafuta na kuifanyia mabadiliko sarafu ya Naira mwaka mmoja uliopita ili kuboresha uchumi. Maafisa wameonya dhidi ya jaribio lolote la kuiga maandamano ya vurugu ya hivi karibuni nchini Kenya ambako