Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wananchi wa Ngerengere na Morogoro Mjini akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma kwa Usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ngerengere Mkoani Morogoro wakati akielekea Dodoma kwa Usafiri wa Treni ya Kisasa ya (SGR). Mhe. Rais Dkt. Samia amezindua Rasmi huduma za Usafiri wa Treni hiyo kuanzia eneo la Kilometa 0 Stesheni Jijini Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wa Ngerengere Mkoani Morogoro mara baada ya kuwasili kwa Treni ya Kisasa (SGR) wakati akitokea Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye Treni ya Kisasa (SGR) katika Stesheni ya Ngerengere Mkoani Morogoro tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Morogoro katika eneo la Stesheni ya Morogoro wakati akielekea Dodoma kwa Usafiri wa Treni ya Kisasa ya (SGR). Mhe. Rais Dkt. Samia amezindua rasmi huduma za Usafiri wa Treni hiyo kuanzia eneo la Kilometa 0 Stesheni Jijini Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Mkoani Morogoro kwa Treni ya Kisasa (SGR) tarehe 01 Agosti, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia amezindua rasmi huduma za Usafiri wa Treni hiyo kuanzia eneo la Kilometa 0 Stesheni Jijini Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.