RISASI imekuwa kinara kwenye msimamo wa mashindano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Shinyanga ikizikimbiza timu nyingine kwa kuwa na pointi tisa.
Ligi hiyo ambayo imeanza mzunguko wa pili, Risasi inafuatiwa na Kahama Sixers yenye pointi saba, huku B4 Mwadui ikiwa na sita na Veta tano.
Kwa mujibu wa Kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi hiyo, George Simba alisema ligi hiyo inachezwa nyumbani na ugenini na mshindi wa kwanza baada ya mzunguko wa pili atacheza na timu itakayoshika nafasi ya nne katika hatua ya nusu fainali.
Alisema timu itakayoshika nafasi ya pili itacheza na timu itakayoshika nafasi ya tatu na mfumo utakaotumika ni wa kucheza ‘best of three play off’.