SERIKALI YATANGAZA MPANGO WA KUWEKA KAMERA ZA UCHUNGUZI 6,500 KATIKA MAJIJI MAKUU – MWANAHARAKATI MZALENDO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, ametangaza mpango wa Serikali wa kuweka mitambo ya kamera za uchunguzi 6500 katika Majiji makuu manne kama hatua ya kwanza katika kupambana na uhalifu na kuboresha usalama wa wananchi.

Sillo alitoa taarifa hii wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kagera, ambapo alikutana na Taasisi zinazoshughulika na usalama kama Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Katika mkutano huo, alisikiliza changamoto wanazokutana nazo na kujadili hatua za kuzikabili.

Amesema kuwa mitambo hii ya kamera itasaidia kutambua na kukamata wahalifu na kuongeza ulinzi katika maeneo yenye watu wengi kama masoko, viwandani, na kwenye makampuni, na pia katika Majiji makuu ya Arusha, Mwanza, Dodoma, na Dar es Salaam.

Sillo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuimarisha vyombo vya usalama, akiongeza kuwa mradi huu wa “Majiji Salama” utaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo haya kwa kuanzia na awamu hii ya kwanza ya kamera 6500.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts