Shilingi Trilioni 3.2 zasainiwa kuanzisha kiwanda cha chakataji wa mbolea

Kituo cha uwekezaji nchini TIC, na Mamlaka ya usimamizi wa mbolea TFRA pamoja na shirika la maendeleo la nishati ya gesi na mafuta TPDC zimesaini hati ya makubalian na Kampuni ya PT Essa ya nchini Indonesia yenye thamani ya shilingi trilioni 3.2 kwa ajili ya uanzishaji wa kiwanda cha chakataji wa mbolea aina ya yurea inayotumia malighafi ya gesi asilia.

Akishuhudia kusainiwa kwa makubaliano hayo , waziri wa nchi ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kiwanda hicho kitasaidia nchi kupunguza uagizaji wa mbolea nje ya nchi kwa asilimia 100 na kuchagiza shughuli za kilimo akiweka bayana kuwa kwa sasa nchi inazalisha mbolea kwa asilimia 10 huku asilimia 90 ikiagizwa kutoka nje.

Mhe. Prof. Kitila Mkumbo alisema kuwa MOU imefanya hatua muhimu katika kuongeza uwezo wa Tanzania katika kilimo, kuhakikisha usalama wa chakula, na kukuza uchumi.

Mradi huu wenye  thamani ya Shilingi trilioni 3.2 za Kitanzani unatarajiwa kuzalisha tani milioni 1 za mbolea kila mwaka
na kutoa ajira 389,000 huku ukiutarajiwa kufanya kazi kikamilifu hadi mwaka 2029.

Mhe. Prof. Mkumbo alisisitiza kuwa mpango huu kabambe ni matokeo ya moja kwa moja ya ziara ya Rais Samia Suluhu mwezi Januari nchini Indonesia, akisisitiza dhamira ya mataifa yote mawili kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na uwekezaji

Related Posts