*Yaahidi kukuza viongozi wa baadaye kupitia mpango huo wa mafunzo.
*Programu imebadilika kuwa ya miezi 12 kwa mafunzo maalum.
Asilimia 93 ya uhifadhi, kuimarisha uongozi wa kibenki na athari chanya kwa sekta za fedha.
Dar es Salaam, Tanzania – Jumatano, 31 Julai 2024 – Benki ya Stanbic Tanzania imetangaza kuhitimu kwa kundi la vijana waliopata mafunzo kupitia mpango wake wa hivi karibuni wa kuwaendeleza kwenye sekta ya kibenki, mpango huo wa kipekee uliokuwa na lengo la kukuza na kuendeleza kizazi kijacho cha viongozi katika sekta ya kibenki. Huu ni mpango unaosisitiza kubadilisha hali na dhamira ya Benki ya Stanbic Tanzania katika kukuza talanta za ndani na kuleta ubunifu katika sekta ya fedha.
Tangu kuanzishwa kwake, programu ya mafunzo ya Vijana wa Benki ya Stanbic Tanzania wamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mtandao wa ndani wa talanta wa kibenki. Wahitimu wa mafunzo haya kwa asilimia 93% wanabaki katika ajira ya benki na kukuza talanta bora. Wahitimu kutoka kwenye mafunzo ya mwanzo, kama Mise Chikoma, ambaye sasa ni Meneja wa Ufahamu wa Wateja, na Natasha Mbaga ambaye ni Meneja wa Mahusiano katika Benki ya Stanbic Uganda, wanathibitisha mafanikio ya mpango huu katika kujenga uongozi wenye nguvu.
Rabina Masanja, Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo alisisitiza umuhimu wa mpango huu, alisema, “Tunajivunia sana mafanikio tuliyopata kutoka kwenye makundi yetu ya mwanzoni. Hadithi zao za mafanikio ni ushahidi wa ufanisi wa mpango huu na dhamira yetu ya kukuza talanta za kiwango cha juu.”
Bw. Manzi Rwegasira, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, alielezea furaha yake ya mpango huu, alisema, “Tunaposherehekea kuhitimu kwa kundi hili, tunatarajia pia utekelezaji wa mfano mpya wa miezi 12 kwa makundi yajayo. Mabadiliko haya yamekusudiwa kutoa mafunzo ya hali ya juu kwa wahitimu wetu na kuharakisha ujumuishaji wao katika majukumu muhimu. Tunaamini kuwa mafunzo haya yatawafaidisha wahitimu wetu lakini pia utaongeza thamani kubwa kwa benki.”
Wahitimu hawa wamepata uzoefu kwa vitendo katika idara mbalimbali kwa kuwaandaa kwenye majukumu muhimu ndani ya benki. Kundi la wahitimu lilionyesha uvumilivu, ubunifu na dhamira ya ubora mkubwa katika kipindi chote cha miezi 18 ya mafunzo. Wahitimu wameonyesha utayari wao wa kutoa mchango wa Benki ya Stanbic Tanzania na sekta ya fedha kwa ujumla.
Katika hotuba yake, Bw. Rwegasira aliendelea kuhamasisha wahitimu, “Mnapoingia katika majukumu yenu mapya, ninawasihi mkumbatie ubunifu na kujifunza mara kwa mara. Safari yenu katika Benki ya Stanbic Tanzania imeanza, na nina imani kwamba mtatoa mchango mkubwa, si tu kwa benki yetu, bali kwa sekta ya kifedha kwa ujumla.”
Benki ya Stanbic Tanzania inaendelea na dhamira yake ya kukuza na kuendeleza talanta za kiwango cha juu ndani ya benki.