Dar es Salaam. Treni ya reli ya umeme (SGR) kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ikiwa na abiria na wageni mbalimbali wakitoka kushiriki uzinduzi wa treni hiyo imekwama kwa muda mkoani Morogoro jana Alhamisi Agosti 1, 2024.
Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:”Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa.”
Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:”Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani.”
Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.
Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC)