Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo Dk Bill Kiwia amewataka wanafunzi kujitokeza zaidi kuomba mkopo kabla dirisha halijafungwa huku zikiwa zimebaki siku 30 ambapo ni sawa na mwezi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari Dkt.Bill amesema wanafunzi wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo huku wakitakiwa kufuata miongozo iliyowekwa na bodi katika kuomba mkopo
Kwa mujibu wa bodi ya mikopo hadi sasa wameshapokea maombi elfu 40 ya wanafunzi walioomba mkopo,lakini licha ya kusisitiza watu kuomba mkopo,mkurugenzi anakiri kuwepo kwa changamoto ya kufichua wanaodaiwa hadi sasa na hapa wanakuja na mkakati mpya wa mafunzo ili watu waweze kuajiriwa na kujiajiri.
Hata hivyo bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inaendelea kuwakumbusha watanzania kuwa mikopo hiyo ni kwaajili ya wanafunzi wa Bachelor Degree, Diploma,Masters, Phd na kundi la ufaulu wa juu ktk tahasusi za sayansi ambao wataweza kuomba mkopo wa Samia scholarship
#KonceptTvUpdates