WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT. PINDI CHANA AZINDUA KITUO CHA MAWASILIANO KWA AJIL YA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Katika hatua kubwa ya kuimarisha utatuzi wa migogoro nchini, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Pindi Chana, ameanzisha kituo cha mawasiliano “contact center” maalumu kwa ajili ya wananchi kuwasilisha migogoro yao moja kwa moja wizarani.

Dkt. Chana amepongeza juhudi za serikali katika kutatua kero na migogoro kwenye jamii, na amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wananchi wanapata haraka ufumbuzi wa migogoro hiyo. Kituo hicho kitakuwa chini ya usimamizi wa wataalamu waliopo wizarani ambao watahakikisha kila mgogoro unaowasilishwa unapokelewa na kushughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi.

Aidha, amewataka viongozi mbalimbali kutumia kituo hiki katika kusuluhisha na kutatua migogoro ya wananchi kwa mujibu wa sheria. Amehimiza wananchi kutumia namba “0262160360” ili kuwasilisha migogoro yao na kupata ufumbuzi wa haraka.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts