WIMBO MPYA WA HARMONIZE GUMZO MITAANI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Msanii na staa wa Bongo Flavour Tanzania, Harmonize, ametambulisha wimbo mpya wa Yanga (Yanga Hii Unaifungaje), atakao tamba nao siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi katika dimba la Benjamin Mkapa.

Wimbo huo umeonekana kuwa ni bora kati ya nyimbo zote alizoziimbia timu yake huku mwenywe akidai kuwa Wiki ya Mwananchi ya msimu huu itakuwa bora sana kwake.

Aidha Harmonize amekili kuwa ni bahati kwake ni heshima kubwa san kualikwa katika tamasha kama hilo kwa mara ya pili sasa. Ikumbukwe kuwa mara ya kwanza alialikwa arishuka kama komando wa vita katika dimba hilo, tutegemee makubwa zaidi katika siku hiyo ambayo itakuwa ni Jumapili ya tarehe 4 mwezi 8.

#KonceptTvUpdates

Related Posts