KOCHA wa Azam FC, Youssouph Dabo amemaliza mafunzo na kuliwahi pambano la Tamasha ya Rayon Sport linalofanyika kjijini KIgali, Rwanda likienda kwa jina la Azamka in Rwanda, huku akitamba kwamba kila kitu alikuwa anakijua na kwamba mashabiki wa timu hiyo wasubiri burudani kesho Jumamosi.
Dabo aliondoka kambi ya Azam iliyokuwa Morocco ili kuja kupiga brashi ya ujuzi kwa lesei yake ya ukocha katika ngazi ya daraja la juu zaidi kwa CAF (Diploma A), iliyofanyikia Tanga na ameshamaliza, huku akisema yupo tayari kuendeleza kile alichofanya Bruno Ferry ikiwamo mechi ya leo jijini Kigali.
Kwa sasa Dabo atakuwa akitambulika kama kocha mkuu tofauti na awali licha ambapo alikuwa msaidizi, kutokana na kukosa vigezo alivyopata kwa sasa baada ya kuingia darasani kusoma.
“Nalishukuru Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kutoa nafasi ya makocha kusoma, tayari nimemaliza kozi kwa sasa najiona nina deni, kuhakikisha naisaidia timu kufanya vizuri zaidi ya mwakajana ambapo tulimaliza nafasi ya pili,” alisema Dabo na kuongeza;
“Wakati timu ipo Morocco, nilikuwa napewa ripoti ya kila siku, baada ya kumaliza kambi hiyo, nimepewa ripoti ya jumla, iliyonipa picha ya kipi kitakwenda kufanyika msimu ujao.”
Dabo alisema ukubwa wa kambi hiyo, umeongeza kujiamini kwa wachezaji, jambo analoliona litawasaidia kufanya vitu vikubwa, Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Timu ilicheza mechi za kirafiki na timu nzuri, hilo lilikuwa jambo kubwa kwa wachezaji wetu kujengewa kujiamini na limewapa nguvu ya kukabiliana na kila timu tutakayokutana nayo kwenye michuano mbalimbali,” alisema Dabo, huku kocha wa Rayon Sports ya Rwanda, Mbrazil Roberto Oliviera ‘Robertinho’ aklisema anatarajia kupata kipimo kizuri kuitoka kwa Azam iliyomaliza nafasi ya pili Ligi Kuu Bara iliyopita ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikipangwa kuvaana na APR pia ya Rwanda.
“Naamini tutakuwa na wakati mzuri wa kujipima dhidi ya Azam FC, moja ya timu nzuri na bora kwa Tanzania, tupo tayari kuwapa changamoto, kwangu ni nafasi ya kuendelea kukijenga kikosi changu,” Robertinho aliyewahi kuinoa Simba kabla ya kutimuliwa baada ya kipiogo cha 5-1 kutoka kwa Yanga.