Mbunge Mlimba ashauri kutolewa mikataba ya muda ajira za afya

Mbunge wa Jimbo la Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro Godwin Kunambi ameishauri serikali ya Wilaya hiyo kutoa ajira za mikataba ya muda Kwa wafanyakazi wa kada ya afya Ili kukabiliana na Changamoto hiyo.

Mhe. Kunambi ameyasema hayo wakati wa mahafali ya Tano ya Chuo Cha Afya na sayansi Shirikishi Mlimba ambapo amesema njia pekee ya kukabiliana na Changamoto hiyo ni kutoa ajira za muda kwa wanafunzi wanaohitimu katika Chuo hicho na Maeneo mengine nchini.

Kunambi amesema Serikali imetoa zaidi ya Shilingi bilioni Moja Kwa ajili ya ujenzi wa majengo vya kutolea huduma za afya katika eneo hilo na Sasa kuna vituo vya afya zaidi ya vitano na hospitali ya Halmadhuri ya Wilaya vyote vimekamilika na kuanza kutoa huduma lakini Changamoto upungufu wa wataalam.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Mlimba akiwemo Juma Mrisho na Jane Mputu wamesema wanaishukuru serikali Kwa kuendelea kujenga majengo ya kutolea huduma za afya ombi lao ni kupatiwa vifaa tiba,wataalam na Madawa.

Mkuu wa Chuo hicho cha Afya Mlimba Jameson Kiengela amesema lengo la kuanzishwa kwa Chuo hicho katika mazingira hayo ni kukabiliana na Changamoto hiyo ya wahuduma wa afya ambapo ameushuruku uongozi wa Kituo cha Afya Mlimba kwa kuendelea kuwatumia wanafunzi katika kutoa huduma kituo hapo.

Related Posts