Asha Athuman, mwanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ameibuka mshindi wa tuzo za Tulia Trust Journalism Awards kwa mwaka 2023/24.
Asha alishindania tuzo hizi katika kipengele cha uandishi wa habari za madini na gesi, zinazohusu mkoa wa Mbeya. Tuzo hizi, ambazo ni sehemu ya juhudi za kutambua na kuhamasisha ubora katika uandishi wa habari, zilitolewa jana usiku katika ukumbi wa Tughimbe, mkoani Mbeya.
Ushindi wa Asha Athuman unafungua milango zaidi ya ufanisi na ubunifu katika taaluma ya uandishi wa habari, hasa katika maeneo ya madini na gesi ambayo yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya taifa.
Tuzo za Tulia Trust Journalism Awards zinatambua kazi bora za waandishi wa habari ambao wameonesha ubunifu na umahiri katika uandishi wa habari zinazohusiana na rasilimali za madini na gesi, huku zikileta mwangaza katika masuala muhimu ya kijamii na kiuchumi
#KonceptTvUpdates