Ni Agosti 2, 2024 ambapo Mke wa Joseph Kusaga aitwae Juhayna Ajmy ametambulisha rasmi Radio yake iitwayo Malkia Choice FM 102.5.
Akizungumza katika Sherehe za uzinduzi huo uliofanya katika hoteli ya hyatt Jijini Dar es Salaam alisema..’Malkia Choice FM ni kituo cha kwanza cha redio kinachoongozwa na wanawake nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, lengo kuu ni kuwezesha na kuonyesha kazi mbalimbali za wanawake kote duniani ikiwemo masuala ya kifedha, kiuchumi, kisiasa, na kijamii ili kuongeza kasi na ubora kwenye maendeleo yetu na taifa letu kwa ujumla’- Juhayna Ajmy Mkurugenzi mtendaji wa Malkia Choice Fm 102.5
Aidha katika Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Radio, wasanii wakiwemo naWaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ambae alikuwa ni mgeni rasmi.
Hizi ni baadhi ya picha zitazame namna Shughuli hiyo ikiendelea muda huu kutoka Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.