SIMBA SC YAMNASA MOUSSA CAMARA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Simba SC imemtambulisha golikipa Mguinea, Moussa Camara akitokea Horoya AC atayeziba pengo la Ayoub Lakred amabaye amepata majeraha yatakayomweka benchi kwa muda mrefu kidogo.

Moussa Camara (alizaliwa 27 Novemba 1998) ni mchezaji wa kandanda wa Guinea ambaye alikuwa anacheza kama kipa wa Horoya na timu ya taifa ya Guinea, sasa ni mali halali ya Simba SC.

Ujio wa Moussa Camara unaacha maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa Simba SC kuhusu uwezekano wa Aishi Salim Manura kusalia katika kikosi hicho. Nyota ambaye amehudumu katika Simba SC kwa mafanikio tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Azam FC.

Kazini kwa Ally Salim kumeongezeka kazi, kutokana na uwezo alionao Moussa huenda ikawa ni changamoto kwake itakayomfanya kuongeza bidii ili kumuanisha kocha kuwa anaweza kubaki katika kikosi cha kwanza.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts