Srelio yazipigia hesabu timu kongwe

KOCHA msaidizi wa Srelio, Miyasi Nyamoko amesema anazipigia mahesabu timu tano kongwe zinazoshiriki ligi ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).

Miyasi ambaye pia ni mchezaji wa timu hiyo, alizitaja timu hizo ni JKT, Savio, ABC, Mchenga Star na UDSM Outsiders.

Alisema wakishinda dhidi ya baadhi ya timu hizo, watakuwa katika nafasi ya nne bora.

“Kama tuliifunga Dar City, Vijana ‘City Bulls’ na Pazi kwa nini tusishinde,” aliuliza Nyamoko.

Akizungumzia timu zingine ambazo hawajacheza nazo kama  Crows, Mgulani (JKT), Jogoo, Chui na Ukonga Kings, ametamba haziwezi kuwasumbua.

“Kwa kweli sasa timu yangu iko vizuri, tumejipanga  kupambana hadi mwisho,” alisema Nyamoko.

Related Posts