VIJANA Queens imeishusha DB Troncatti katika nafasi yake ya uongozi wa ligi hiyo kwenye msimamo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam.
Vijana sasa inaongoza msimamo huo ikiwa na pointi 38 ikifuatiwa na DB Troncatti yenye 38 zikitofautiana kwa idadi ya kufunga vikapu, Vijana ikiwa na 1470, huku DB ikifunga 1439.
Timu ngeni katika mashindano hayo, Tausi Royals inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36, ikifuatiwa Pazi Queens iliyopata pointi 35, DB Lioness (34), Jeshi Stars (30), JKT Stars (31), JKT Stars (30), Polisi Stars (30) na Mchenga Stars (27).
Zingine ni Mgulani Stars (25), Ukonga Queens (25), City Queens (24), Twalipo Queens (21), Kurasini Divas (21), Kigamboni Queens 21 na UDSM Queens (21).
PLP W L PTS
Vijana Queens 20 18 2 38
DB Troncatti 20 18 2 38
Tausi Royals 20 16 4 36
Pazi Queens 21 14 7 35
DB Lioness 20 14 6 34
Jeshi Stars 18 13 5 31
JKT Stars 16 14 2 30
Polisi Stars 20 10 10 30
Mchenga Queens 21 7 13 27
Mgulani Stars 17 8 9 25
Ukonga Queens 19 6 13 25
City Queens 19 5 14 24
Twalipo Queens 17 4 13 21
Kurasini Divas 19 3 15 21
Kigamboni Queens 19 2 17 21
UDSM Queens 20 1 19 21