Zoezi la kupiga kura kuwapata viongozi wa chama cha mawakili TLS linaendelea

Zoezi la kupiga kura kuwapata viongozi wa chama cha mawakili wa Tanganyika (Tanganyika Law Society- TLS) linaendelea hapa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma zoezi hili linaendelea baada karatasi ya kupigia kura kuisha na kwenda kuchapa zingine kwa kinachotajwa kuwa idadi ya wapiga kura kuongezeka.

Zoezi lilianza saa 12:00 asubuhi na karatasi zilikwisha majira ya saa tano asubuhi kabla ya kupatikana zingine saa saba mchana ambapo TLS kupitia ukurasa wao wa X wameandika zoezi hilo limeendelea majira ya saa 07:20 na linatarajia kikamilika saa 08:20 mchana.

Wagombea wa nafasi ya urais utakaodumu kwa miaka mitatu ni Bonface Mwambukusi, Sweetbert Nkuba, Emmanuel Muga, Capt. Ibrahim Bendera, Paul Revocatus Kaunda na Revocatus Kuuli.

Related Posts