ZRA Julai yakusanya Billioni 53.322

Mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA katika taarifa yake ya kwa walipa kodi imesema katika mwezi wa Julai wa mwaka wa Fedha 2024/2025 ikikadiriwa kukusanya Tsh 50.490 Billioni na imefanikiwa kuvuka lengo katika mwezi Julai

akisoma Taarifa hiyo Said Ali Mohammed ambae ni Kaimu Kamishna Mkuu wa ZRA amesema mamlaka ya mapato Zanzibar imefanikiwa kukusanya Tsh 53.322 Billioni ambayo ni sawa na Ufanisi wa asilimia 105.61 ya makusanyo ya mapato yaliotarajiwa kukusanywa

Aidha Makusanyo halisi ya mwezi Julai ya mwaka uliopita wa 2023/2024, yalikuwa ni Tshs 42.898 Bilioni, yakilinganishwa na Makusanyo halisi ya Julai ya Mwaka huu wa”edha wa 2024/2025, yanaonesha ukuaji mkubwa Makusanyo halisi wa asilimia 24.30

Related Posts