Foleni Simba Day balaa! | Mwanaspoti

‘UBAYA UBWELA’ hadi kieleweke zimesikika sauti za mashabiki wa Simba ambao wamekaa katika nguzo za umeme wakisubiri foleni ya kuingia uwanjani.

Nguzo hizo za chuma zimelazwa chini mita chache kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kunafanyika shughuli ya kilele cha tamasha la Simba Day.

Unaambiwa, kutokana na msururu wa mashabiki wengi waliopanga mstari kuingia ndani ya uwanja wengine wakaona wapumzike kidogo kwenye nguzo hizo.

Mashabiki hao wamejazana kwenye nguzo hizo kama sehemu ya kunyoosha miguu baada ya kusimama kwa muda mrefu.
“Ubaya Ubwela hadi kieleweke hatuchoki hii ndio shughuli yetu, tukae tusimame lazima tuingie ndani kuiona Simba yetu mpya,” alisema mmoja wa mashabiki.

Baadhi ya mashabiki wakilalamikia utaratibu mbovu wa kuingia uwanjani, kwani foleni imekuwa kubwa na milango ikiwa imefunguliwa baadhi na kuwapa kero waliojihimu mapema tamashani kupata burudani.

Mashabiki lukuki wakiwa wanje ya uwanja huo wameonekana kukosa subira kwa madai utaratibu unawachosha kabla ya kuingia uwanjani.

Related Posts