Simba Day bado kidogo iwe full house

MASHABIKI wa Simba hawana jambo dogo hivyo unavyoweza kusema baada ya kubakiza kama robo ya uwanja kabla ya kuujaza Uwanja wa Mkapa zikiwa zimebaki saa tano shughuli ya utambulisho wa kikosi kipya cha msimu ujao haujafanyika.

Licha ya nje ya uwanja kuonekana kuwa na mashabiki kibao, ila ndani ya uwanja ni maeneo machache yamebaki ili idadi ya mashabiki 60,000 ikamilike.

‘Ubaya Ubwela’ ambayo ndio kauli inayotamba kwa Mkapa, imethibitishwa na nyomi la mashabiki ambao wanaendelea kuingia mdogo mdogo kutokana na foleni ya kuingia kwenda taratibu.

Simba inatarajia kutambulisha kikosi cha msimu huu saa chache zijazo, ikiambatana na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya APR ya Rwanda.

Mashabiki walioingia ndani ya uwanja wanaendelea kuburudishwa na muziki unaopigwa na Dj kabla ya wasanii waliotajwa kutumbuiza.

Related Posts