BillNass aingia kitofauti kwa Mkapa 

MSANII wa kizazi kipya ‘BillNass’ atua kivingine katika uwanja wa Benjamin Mkapa huku akitoa burudani ili washangaza mashabiki.

Staa huyo alitua na kikundi chake kikiwa kimebeba vitu vilivyoonekana kama Ungo kumbe ni picha za wachezaji wa Yanga.

Huyu ni msanii wa pili kuliamsha katika siku hii ya Wananchi, baada ya kutoka Christian Bella, ambaye nae aliwainua mashabiki ingawa sio sana kutokana na mechi iliyokuwa ikiendelea.

Licha ya hayo nyimbo za Billnas zilionekana kuwapa vaibu Wananchi na kuwafanya kuinuka na kupiga shangwe za kutosha.
Miongoni mwa nyimbo alizozicheza ni pamoja na Puu, Mabosi na Sisi ndio Yanga iliyoimbwa na  Mke wake Nandy, huku akizunguka uwanja mzima kuwapa vaibu wageni na mashabiki kabla ya kuwapisha wakali wengine wa singeli wanaoendelea kutumbuiza kwa sasa.

Related Posts