DJ Ally B akiwasha kwa Mkapa

DJ maarufu nchini, Ally Suleiman Simba ‘DJ Ally B’, amegeuka msanii wa muda mfupi, nje na kazi yake ameamua kuimba nyimbo mbalimbali za wakongwe.

DJ huyo alikuwa anapiga nyimbo na kuimba ambapo alifanya shangwe za mashabiki zilipuke katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika tamasha la kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’.

Ally B, alikuwa anazima muziki aliokuwa akiupiga ukigusa nyimba ya mastaa kibao wa ndani na nje ya nchi, kisha kuimba mwenyewe akishirikiana na mashabiki, jambo lililowafanya wawe na shangwe za hali ya juu, kuimba na kucheza.

Miongoni mwa nyimbo za wasanii alizozipiga ni za Mr Blue, Profesa Jay, Matonya, TID na nyingine kibao na mzuka ulipozidi aliivua jeshi mpya ya Yanga aliyoivaa sambamba na overaroli na kuwarushia mashabiki walioigombea.

Related Posts