MSEMAJI wa Yanga, Haji Manara ameibua shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuhudhuria tamasha la ‘Wiki ya Mwananchi’ akiwa na Mke wake, Zaylissa.
Manara ametua uwanjani hapo ikiwa ni siku chache tangu amalize kifungo cha miaka miwili cha kutojihusisha na masuala mbalimbali ya michezo ndani na nje ya nchi.
Wakati wa kuingia uwanjani hapo, yalionekana magari mawili meusi aina ya Toyota Land Cruiser na ndipo Manara alipotokea akiwa na mkewe.
Kitendo hicho kiliibua shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walionekana kufurahishwa na ujio wake uwanjani hapo.
Manara alifungiwa kutojihusisha na masuala ya michezo Julai 2, 2022 baada ya kukutwa na hatia ya kumdhalilisha Rais wa TFF, Wallace Karia.
Manara ndiye aliyetumika kutambulisha kikosi cha msimu wa 2024-2025 akianza na benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya Kocha Miguel Gamondi.