NYOTA wa muziki wa Bongo Felva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ a.k.a Konde Boy amewapagawisha mashabiki wa timu hiyo wakati wa kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ kilichofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Konde Boy aliingia uwanjani hapo kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wa timu hiyo huku akianza kuimba wimbo wa ‘Yanga Hii Unaifungaje’.
Wimbo huo ulianza kuwaamsha mashabiki huku wakiimba na kucheza kwa pamoja katika sherehe hizo ambazo ni za sita kwa timu hiyo kufanyika tangu zilipoanza rasmi mwaka 2019.
Nyimbo nyingine alizoimba msanii huyo ni pamoja na Tabulele, single again, kushoto kulia, ameloa, disconnect na Sensema ambazo zote zilipokelewa vizuri na mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya Marioo na Rayvanny kujumuika naye na kuliamsha.
Rayvanny aliingia na guta lenye madumu ya mafuta huku akilisukuma mwenyewe, kisha kuliamsha pamoja kwa kuimbisha mashabiki waliokuwa wakiwashangilia muda wote.