Mario asapraizi mashabiki kwa pikipiki

MSANII wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga ‘Marioo’ amewafanyia sapraizi mashabiki wa Yanga kutokana na aina  ya uingiaji wake Uwanja wa Benjamin Mkapa kutumbuiza sherehe za kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Kabla ya msanii huyo kuingia yalianza kupigwa mafakati juu, walifuatilia waendesha bodaboda waliozunguka uwanja akiwamo naye akiendesha yake, jambo ambalo lilifanya mashabiki kupata vaibu la kucheza na kuimba.

Mario aliimba wimbo wa Hakuna Matata ambao ulikuwa na mwitikio mkubwa kwa mashabiki uwanjani hapo.

Wakati anaimba kuna muda mafataki yalikuwa yanapigwa, jambo ambalo mashabiki liliwapa raha na kuanza kucheza kwa pamoja kabla ya kuangusha ngoa kadhaa za kutosha na baadae kumpisha DJ Ally B anayeendelea kuliamsha kwa sasa uwanjani hapo ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano, Dk Philip Mpango ambaye ameshaingia uwanjani kushuhudia burudani za Wananchi..

Related Posts