KIKOSI cha Yanga kimetinga ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, kikiwa kimevaa simpo tu, tofauti na miaka ya nyuma lakini kikiamsha shangwe kwa mashabiki walioujaza uwanja huo katika Tamasha la Wiki la Mwananchi.
Timu hiyo imewasili Uwanja wa Mkapa saa 12:09 Jioni ikiwa na msafara wa magari matatu tu likiwemo basi lao kubwa na pikipiki ya polisi.
Saa 12:30 kikosi hicho kiliingia ndani ya uwanja wamevalia raba nyeupe,Suruali za mazoezi na kaptula huku juu wakiwa wametupia Tshirt zote nyeusi.
Tofauti na miaka ya nyuma ambapo timu hiyo imekuwa ikiingia na vazi la suti zenye mtindo tofauti kuwasalimia mashabiki wao.
Mabingwa hao mara tatu wameungana kikosi kizima ambacho kinajumuisha wachezaji wapya na wazamani, huku wakizunguka uwanja mzima.
Vaibu la mashabiki kila upande ndilo linaloonekana tu, huku nyuso za bashasha ndizo zilizojaa kwa mastaa hao baada ya kuona umati uliojitokeza.
Aidha imekuwa ni desturi kwa wachezaji kuonekana wakati wa kutambulishwa ila hii ya leo ni mpya.
Yanga msimu huu imesajili mastaa kama Clatous Chama, Prince Dube, Duke Abuya, Jean Baleke, Chadrack Boka, Aziz Andambwile na Abubakar Khomeiny ambao wote waliokuwapo wale waliokuwapo msimu uliopita.