Mboto kama Mourinho | Mwanaspoti

MSANII wa vichekesho,  Mboto amejigeuza Jose Mourinho wakati akiiongoza timu ya masupastaa wanaoishabiki Yanga akiwa kama kocha amefanya kituko cha kuamua kuingia uwanjani kumfokea straika baada ya kukosa bao.

Timu hiyo inacheza dhidi ya Maveterani Yanga ambapo timu hiyo ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 aliona isiwe tabu kwa kuamua kuingia uwanjani baada ya mshambuliaji mmoja wa timu hiyo kukosa bao na kumfuata aliposimama na kuanza kumfokea.

Baada ya kumaliza kufoka alitoka ndani ya uwanja, huku akiwa anacheka, jambo lililoonekana linawapa burudani mashabiki jukwaani.

Mechi hiyo ni ya utangulizi ambapo Yanga saa 2:00 usiku itacheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Mashabiki wanafurahishwa na mechi hiyo, kwani upande wa timu ya Maveterani Yanga wapo mastaa wa zamani kama Fredy Mbuna, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ ambao ni kama wanawakumbusha enzi.

Related Posts