MWIMBAJI wa singeli nchini, Meja Kunta ameingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ huku akiimba wimbo maalumu wa timu hiyo unaojulikana kwa jina la Mwananchi aliomshirikisha Billnass.
Wimbo huo uliamsha shangwe kwa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo ambalo walianza kuimba na kucheza kwa pamoja.
Mbali na wimbo huo ila Meja Kunta aliimba nyimbo mbalimbali zikiwemo, demu wangu, nakupenda wewe na huyo bwana ako, sikuachi nakupenda na Hassani ambazo ziliamsha mzuka kwa mashabiki ambao walionekana kufurahishwa na aina ya nyimbo hizo.
Sherehe hizo za kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ zinahitimishwa kwa mchezo wa kirafiki ambao Yanga itacheza na mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia, Red Arrows kuanzia saa 2:00 usiku ikiwa ni msimu wa sita wa tamasha hilo lililoasisiwa mwaka 2019.