RAIS SAMIA AZINDUA DARAJA LA RUAHA, KIDATU – IFAKARA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Rais Samia Suluhu amelizindua rasmi Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 lililopo katika barabara ya Mikumi – Kidatu – Ifakara sehemu ya Kidatu – Ifakara yenye Kilometa 66.9 leo Agosti 4, 2024.

 

 

Daraja hilo limejengwa na mkandarasi wa Reynolds Construction Company ya Nigeria na mhandisi mshauri ametoka TANROADS Engineering Consulting Unit – TECU.

 

 

Daraja hilo limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu – Ifakara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kuanzia tarehe 2 Oktoba 2017 na umekamilika tarehe 30 Juni, 2024 huku ukigharimu Shilingi Billion 157.15 zilizohusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Related Posts