Tanzania imara mbio za kufuzu Kombe la Dunia

TIMU ya taifa ya vijana ya Kriketi imeanza vyema mbio za kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa vijana walio chini ya miaka 19 kwa Divisheni ya Pili baada ushindi mnono wa wiketi 6 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Dar Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Ni timu tatu kati ya nane zinashiriki ndiyo zitakata tiketi ya kucheza fainali na hivyo kupanda daraja hadi kuwa divisheni ya kwanza. 

Ili kuwa na uhakika wa kufuzu, Tanzania inahitaji kushinda mechi mbili zilizobaki ambazo zitaipeleka katikla nafasi ya nne bora ambayo baadaye itatoa washiriki watatu wanaostahili kupanda daraja.

Tanzania ilianza vizuri mbio za kusaka tiketi ya kufuzu fainali baada kuifunga Nigeria kwa wiketi 6 katika mechi ya ufunguzi uliyochezwa katika uwanja wa Dar Gymkhana mwishoni mwa juma.

Vijana wa Nigeria ndiyo walionza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio 127 baada ya wote kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 45 kati ya 50 ya mchezo huo.

Kazi ya kuifukiza mikimbio hiyo haikuonekana ngumu sana kwa Watanzania kwani waliweza kuifikia na kuipita kwa kutengeneza mikimbio 128 huku wakipoteza wiketi 4 tu.

Walishinda wakitumia mizunguko 35 kati ya 50 iliyowekwa.

Augustine Mwamele aliyeshinda wiketi 3, Laksh Bekrania aliyeshinda pia wiketi 3 na Ally Hafidh Ally aliyeshinda wiketi 2, ndiyo walioibeba Tanzania dhidi ya wapinzani wao.

Kwa upande wa Nigeria  wachezaji Femi Oresenwo aliyetenghenza mikimbio 26 na Ali Rahmon aliejazia mikimbio 20, ndiyo waliofanya vizuri ingawa mikimbio waliyoitengezea haikufua dafu kwa Watanzania.

Katika uwanja wa UDSM jijini, Ghana iliwafunga Msumbiji kwa wiketi 4 katika mchezo mwingine wa ufunguzi.

Msumbiji ndio walioshinda kura ya kuanza na jitihada zao zikawafikisha kwenye mikimbio 80 baada ya wote kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 34 kati ya 50 iliyopangwa.

Iliwachukua vijana wa Ghana mizunguko 11 tu kuwapiku wapinzani baada ya kutengezeza mikimbio 81 huku wakipoteza wiketi 6.

Mcheza Lee Nyarko ndiye alikuwa shujaa kwa upande wa Ghana baada ya kuangusha wiketi 5 za wapinzani peke yake. Benard Ado na  David Ateak nao walipata wiketi 2 kila mmoja.

Timu nyingine zilizoanza vyema mashndano haya ya kufuzu ni Botswana ambao waliwafunga Malawi  kwa mikimbio 61 katika mchezo wa kundi B uliocjezwa uwanja wa Dar Gymkhana sikuya Jumamosi.

Botswana ndio walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio 149 baada ya wote kutolewa wakiwa wamefikisha mizunguko 47 kati ya 50 iliyopangwa.

Jitihada za vijana wa Malawi ziligota kwenye mikimbio 88  wakitumia mizunguko 23.5 kati ya  50.

Ayush Harith wa Botswana ndiye aliyekuwa nyota wa mikimbio baada ya  kuipa timu yake mikimbio 32 pele yake.

Katika mchezo mwingine wa kundi B, Sierra Leone waliifunga Rwanda kwa wiketi 7 kwenye Uwanja wa UDSM  uliochezwa jana Jumamosi.

Rwanda waliopata kura ya kuanza waliweza kutengeneza mikiumbio 51 tu baada ya wote kutolewa na kuwapa vijana wa Sierrea Leone kazi nyepesi ya kutumia mizunguko 12 tu kuzifikia alama zilizotengenezwa na Rwanda huku wakipoteza wiketi 3.

Related Posts