YANGA imeendelea kufanya vizuri kila kona baada ya kikosi hicho cha Maveterani kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Wasanii, katika mchezo wa utangulizi kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi.
Hizi zote ni shamra shamra za kuchangamsha siku ya Wananchi, huku mechi hiyo ikiwaacha mashabiki na vicheko maana licha ya ushindani mkubwa uliokuwepo vimbwanga huku navyo havikukosekana.
Mechi hiyo iliyochezwa ndani ya dakika 90, bao la kwanza lilifungwa na msanii Fobi lakini baadae Yanga waliamka na kuanza kuuwasha moto mpaka kocha wa timu ya Wasanii kuingia uwanjani baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi na kushindwa kufunga bao.
Wakati wa mchezo huo ukiendelea kipindi cha kwanza aliingia Mtumbuizaji mashuhuri Christian Bella na kufanya mashabiki wa Yanga kupata burudani mara mbili.
Viongozi walioshiriki katika mechi upande wa Yanga ni pamoja na Makamu wa Rais wa kikosi hicho Arafat Haji ndiye aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho cha maveterani na maofisa wa Yanga dhidi ya masupastaa waliongozwa na kina Yusuf Mlela na wengineo.