ZAIDI YA BILIONI 200 ZINATARAJIWA KUTUMIKA KUPANUA BANDARI YA MTWARA ENEO LA KISIWA MGAO

Elizabeth Msagula,Lindi

Zaidi ya shilingi bilioni 200 zinatarajiwa kutumika na mamlaka ya bandari Mtwara kwa ajili ya upanuzi na kuongeza utoaji wa huduma wa mamlaka hiyo katika eneo la kisiwa mgao mkoani mtwara.

Hayo yamebainishwa mkuu wa idara ya masoko bandari ya Mtwara na faraji hassan alipokuwa akitoa maelezo ya shughuli za mamlaka hiyo kwa wakuu wa wilaya ya Masasi na Newala Mkoani Mtwara walipotembelea katika banda la mamlaka hiyo katika maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea katika viwanja vya ngogo huko Manispaa ya Lindi.

Amesema ujenzi wa bandari hiyo utakapokamilika itakuwa mahususi kwa ajili ya kusafirishia shehena chafu na hatarishi kama vile pembejeo za kilimo na makaa ya mawe.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi LEUTERI JOHN KANONI ameeleza bandari hiyo inamchango na umuhimu mkubwa katika kuinua uchumi wa wananchi wa mikoa ya kusini huku mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaj MWANGI RAJAB KUNDYA kiishauri mamlaka hiyo kuanza kufikiria kusafirisha mazao ya ufuta na mbaazi katika bandari hiyo.

Related Posts