BARRICK RUNNERS NDANI YA SERENGETI ANTI-POACHING RUN 2024

Mfanyakazi wa Barrick,Safarani  Msuya akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Serengeti,Angelina Marco

Wafanyakazi wa kampuni ya Barrick nchini kupitia klabu zao za mchezo wa Marathon wameshiriki katika mbio za  kilomita 12  za Serengeti Anti-poaching Run 2024 zilizofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara.

 

Wakimbiaji kutoka Barrick Runners clubs wamekuwa wakishiriki marathon mbalimbali zinazofanyika nchini na nje ya nchi.

Kampuni imekuwa na programu za mazoezi kwa ajili ya wafanyakazi wake kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na nguvu na afya bora pia imewekeza katika miundombinu ya michezo na mazoezi kwa ajili ya  kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki michezo na mazoezi katika mazingira rafiki.

Related Posts