Kampuni ya Koncept Group inayojishughulisha na matangazo ya kidijitali, masoko na mahusiano ya umma nchini imeadhimisha kumbukumbu ya miaka 9 ya ufanisi, baada ya kufanilkiwa kuchochea ukuaji wa chapa (brand) mbalimbali nchini.
Kampuni hiyo yenye makao makuu jijini Dar es Salaam imepanga kupanua wigo wake nje ya Tanzania kwa kufungua ofisi mpya huko jijini Dubai kabla ya mwisho wa mwaka huu ambayo itaiwezesha kuingia katika soko Falme za Kiarabu (UAE) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wake wa ukuaji.
Akizungumza katika sherehe za miaka 9 ya kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Koncept Group Krantz Mwantepele alisema kampuni hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza ubunifu na biashara nchini.
Mwantepele alisema kampuni hiyo imeendelea kujiimrisha ili kukidhi mahitaji ya wateja hali ambao imeifanya kampuni yake kuendelea kuwa juu nchini, kutokana na mikakati yake madhubuti na ya kipekee ya masoko na mahusiano ya umma.
“Miaka 9 iliyopita imekuwa ya mafanikio makubwa sasa kwa kampuni yetu ya Koncept Group. Tunashukuru kwa imani ambayo wateja wetu wameweka kwetu na kazi ya kipekee ambayo timu yetu imetoa. Tunafurahia siku zilizopo mbele yetu na tunatarajia kuendelea kuvuka mipaka, kwa kutumia takwimu na teknolojia ili kuwezesha chapa (brand) kustawi kote nchini Tanzania na katika ngazi ya kikanda.” Alisema.
Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyikazi wa kampuni hiyo wa zamani na wa sasa kwa kujitolea kwa nguvu zao zote bila kuyumba hata katika nyakati ngumu.
“Tunapoanza safari ya mwaka wa kumi, tutaendelea kujitolea kuboresha mahusiano ya umma yanayojikita na takwimu, masoko kwa kuzingatia mising endelevu ya biashara. Kampuni yetu itaendelea kuwa mfano mzuri wa jinsi mtazamo wa kufikiria mbele unavyoweza kuleta mapinduzi katika tasnia yetu na kuacha alama ya kudumu,”
Mwantepele alibainisha kuwa kutokana na ukweli kuwa vyombo vya habari vya kidijitali vinaendelea kuleta upinzani kwa vyombo vya habari vya kitamaduni, kampuni yake imeanza utekelezaji wa mkakati wake kabambe wa ubunifu wa bidhaa ambao utasaidia kukuza chapa za wateja wake na kuongeza ushirikishwaji.
“Tutaendelea kuzingatia maeneo matatu muhimu ambayo ni kukuza sifa ya wateja, kujenga chapa zao, na kutoa matokeo ya biashara yenye mafanikio,” alisisitiza.
Akizungumzia kutambuliwa kama mmoja wa “Viongozi 10 wa Biashara Wanaowezesha Zaidi barani Afrika wanao fuatiliwa Mwaka 2024, Mwantepele alisema, “Hii ni heshima kubwa kwangu na inayochochea dhamira yangu ya kuendelea kuleta mabadiliko chanya”
Koncept Group ni muungano wa kampuni mbalimbali za kiTanzania zikiwemo vyombo vya habari, mahusiano ya umma, masoko ya kidijitali, teknolojia, bima, nyumba na makazi (real estate), usafiri wa anga, nishati, biashara ya kilimo, na vifaa vya kielektroniki.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya Koncept Group Krantz Mwantepele (Kulia) akikata keki kama ishara ya kuadhimisha miaka 9 ya kampuni hiyo wakati wa hafla iliyofanyika katika ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Rasilimali Watu na Sheria wa kampuni hiyo Glory Msuya. Picha Mpiga Picha Wetu.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu kampuni ya Koncept Group Krantz Mwantepele (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 9 ya Kampuni hiyo Jijini Dar es salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Koncept Group Krantz Mwantepele (kulia) akimlisha keki Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano na Mikakati ya kidijitali ya Kampuni hiyo Mahatma Ulimwengu (kushoto) wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 9 ya kampuni hiyo Jijini Dar es salaam. Picha kwa staff photographer.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Koncept Group Krantz Mwantepele (mwenye koti, katikati) akiwa katikati picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 9t ya Kampuni hiyo Jijini Dar es salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.