MAENDELEO YA RAIS SAMIA YAPATA SIFA NYINGI IFAKARA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mbunge wa jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro Abubakar Asenga (CCM), amesifu juhudi na maendeleo yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, akisema kwamba haya maendeleo hayajawahi kufanyika tangu dunia iumbwe.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Ifakara wilayani Ifakara mkoani Morogoro siku ya Jumatatu, Agosti 5, 2024, wakati wa Ziara ya Rais Samia, Asenga alisema kuwa wananchi wa Ifakara walihitaji mradi wa maji na sasa mradi wa maji wa Kiburubutu unajengwa.

“Asenga alisema, ‘Ifakara mlisema hapo mradi wa maji tunataka, tangu Nyerere kuna mradi wa maji wa Kiburubutu. Mheshimiwa Rais amemtuma Waziri Aweso, Aweso tumekwenda naye mpaka kwenye mto wenye mamba Lumeno akavuka, bilioni 41 leo tunajenga mradi wa Kiburubutu, tunajenga hatujengi?’

Asenga pia alisisitiza kuwa tangu mwaka 2013, Ifakara haijawahi kupata barabara ya mtaa ya lami hata kilomita moja. Hata hivyo, kwa sasa barabara za lami zenye urefu wa kilomita moja zimejengwa katika tarafa zote za Ifakara, ikiwemo maeneo ya Saint Francis, Sokoni, na Kibaoni.

Rais Samia Suluhu Hassan aliendelea na ziara yake mkoani Morogoro, akifanya juhudi za kusikiliza na kujibu mahitaji ya wananchi huku akihamasisha maendeleo zaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts