Mikoa Saba yafikiwa na msaada huduma za Kisheria

*katika kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Dodoma

WIZARA ya Katiba na Sheria imesema kuwa katika kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia katika Mikoa Saba wameweza kuhudumia wananchi zaidi ya 400,000

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Kaimu wa Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria wa Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema Wizara imejipanga kutoa huduma za Msaada wa Kisheria Mikoa yote nchi katika kuhakikisha wananchi wasio na uwezo kutafuta mawakili wanapata haki zao.

Amesema kuwa katika kutoa huduma hizo wameweza kusajili vyeti vya kuzaliwa kupitia RITA

Hata hivyo amesema ndani Siku Nne katika Maonesho ya Nane Nane wamehudumia wananchi 2096 hivyo ni mwitikio mkubwa wa msaada wa huduma kisheria katika kampeni hiyo.

“Tumejipanga katika kampeni Msaada wa Kisheria ya Samia Legal Aid inatoa matokeo chanya katika kufikia wananchi pamoja na kutatua migogoro”amesema Msambazi.

Kaimu Mkurugenzi wa Msaada wa  Huduma za Kisheria wa Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi  akizungumza na  Waandishi wa Habari kuhusiana walivyoweza kufikia wananchi katika kutoa huduma za Msaada wa Kisheria , kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Related Posts