RAIS SAMIA AMALIZA KERO YA MAJI RUAHA-KILOMBERO – MWANAHARAKATI MZALENDO

WAZIRI wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema Wizara inaleta Shilingi Milioni 500 kukamilisha mradi mkubwa wa maji katika eneo la Ruaha lililopo katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Mradi huu ni ahadi ya Mhe Rais Samia kwa wana Ruaha alipofanya ziara katika eneo hilo na kupokea changamoto kubwa ya Maji waliokua wanapatia wana Ruaha.

Waziri Aweso ameyasema hayo katika ziara ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan aliposimama na kuwasalimia wananchi wa Ruaha ambapo mbali na hilo pia Waziri Aweso amewataka watumishi wa maji kutowabambikizia bili ya maji wananchi.

Katika eneo la Ruaha Kidodi Serikali inatekeleza mradi wa maji wenye Thamani ya Shs. 4,384,077, 232.50. Mradi umefikia asilimia 75% na kwasasa upo kwenye hatua ya majaribio, kwenye baadhi ya maeneo maji yameanza kupatikana. Pia, Mradi huu unatarajiwa kukamilika tarehe 12/10/2024. na ukikamilika utahudumia zaidi ya wakazi 47,000.

Cc: Wizara ya Maji

#KonceptTvUpdates

Related Posts