RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameweka Jiwe la Msingi kwenye kituo cha biashara za Maziwa Zanzibar
Kituo hicho chenye lengo la kutatua changamoto ya masoko ya maziwa na bidhaa za maziwa kimejengwa kwa udhamini wa TADB kupitia Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa Tanzania (TI3P) kwa kushirikiana na Shirika la Heifer International, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wanachama wa UDCU (Chama cha Ushirika wa Wafugaji wa Ng’ombe Unguja).
Pamoja na malengo mengine ya kukuza sekta ndogo ya maziwa kituo hicho kitajikita zaidi kwenye malengo makuu manne:
✅️ Kukusanya Maziwa kutoka kwa wafugaji
✅️ Kusindika na kuchakata maziwa
✅️ Kutoa mafunzo ya mbinu bora za uzalishaji na uchakataji wa maziwa na bidhaa za maziwa
✅️ Kuuza pembejeo na bidhaa za maziwa.