TLS YALAANI VITENDO VYA UDHALILISHAJI, YAITAKA JESHI LA POLISI KUCHUKUA HATUA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii na taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania kuhusu video iliyosambaa ikimuonyesha mwanamke ambaye anadaiwa kuwa anaishi Yombo Dovya, Dar es Salaam, akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na kundi la wanaume, huku video hiyo ikiandikwa na kurekodiwa.

TLS kimesema tukio hilo linaenda kinyume na sheria za nchi pamoja na maadili na utamaduni wa Watanzania. Chama hiki kimeeleza kutokubaliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa aina yoyote, na kimeitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahalifu wote waliohusika katika tukio hilo na wale waliosaidia kutekeleza vitendo hivyo.

Katika taarifa hiyo, TLS imeeleza kuwa inataka wahalifu wote wakamatwe na kufikishwa mahakamani mara moja ili haki iweze kutendeka. Chama hiki pia kimeonyesha dhamira yake ya kushirikiana na vyombo vya usalama na haki jinai katika kuhakikisha wahalifu hao wanakabiliwa na sheria. TLS imeweka msisitizo kwa kifungu cha 4 (e) cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002), na kinasema kitafuatilia mwenendo wa suala hili kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

TLS pia imeitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa pamoja kupinga udhalilishaji na unyanyasaji, na kuacha mara moja kusambaza video zinazohusu tukio hili ili kulinda haki ya mhanga. Chama hiki kinasisitiza umuhimu wa kuheshimu haki, usawa, na heshima kwa kila binadamu katika jamii yetu.

Katika hali ya kipekee, TLS inasisitiza kuwa vitendo vya kikatili na udhalilishaji vinapaswa kupingwa kwa nguvu zote na hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika ili kuhakikisha haki inatendeka na kulinda utu wa kila mwanajamii.

 

#konceptTvUpdates

Related Posts