WAPO wanaosema ni kabila tu mtu ndio hawezi kuhama, lakini imani ya dini watu wanahama. Wapo wanaohama vyama vya kisiasa na hata kwa ishu ya uraia wapo wanaohama na maisha yakaendelea freshi tu na huko katika ushabiki wa soka mambo nako ni moto, ingawa hutokea kwa nadra sana.
Ndio, kutokana na mchezo maarufu wa soka, uliojizolea sifa kwa mashabiki wengi hapa Bongo wakiwemo wasanii wa aina yote, wamekuwa wanazishabikia timu zao wanazozipenda, lakini baadae walizihama.
Kama inavyoonekana msimu huu na msimu uliopita ambao ulikuwa unafanyika usajili kwa ajili ya Ligi Kuu kuanza, kumezuka na maamuzi ya baadhi ya wasanii kushabikia Yanga wakahamia Simba na wale wa Simba wakihamia Yanga.
Hapa chini ni orodha ya wasanii waliohama kambi na kwenda kushabiki upande wa pili, japo juzi kati uamuzi huo ulimpalia Dulla Makabila aliyekataliwa na mashabiki wa Simba aliowazodoa akiwa Yanga kabla ya kuhamia Msimbazi na kama utani mwamba alikosa shoo ya tamasha la Simba Day.
Mwimbaji huyo wa muziki wa Bongo fleva, ambaye hapo awali alikuwa timu ya Yanga na alishawahi kutumbuiza siku ya Yanga Day.
Lakini msimu huu wa Simba Day, Chino Kidd ameibukia Simba na kutumbuiza Kwa Mkapa juzi Jumamosi sambamba na wakali wengine akiwamo AliKiba, Tundaman, Twanga Pepeta na Joh Makini.
Ni mrembo aliyewahi kuwa mke wa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, kwa sasa ni anaigiza tamthilia akitamba na Mawio inayoongozwa na Gabo Zagamba.
Rushayna hapo awali alikuwa akiishabikia Yanga, lakini msimu huu ameonekana akiishabikia Simba na siku ya Simba Day ameposti kwa akaunti yake ya Instagram ameonekana katika picha amevaa uzi wa Msimbazi na kuandika maneno haya ‘Unamjua Simba…Uzi umenyooka kabisa’
Supastaa wa Bongo Fleva nchini na mwanasoka aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali jijini Dar es Salaam kabla ya kusajiliwa na Coastal Union ya Tanga,. Huyu mwamba anafahamika kuwa ni Yanga lialia, lakini amekuja kugeuka na kuwa shabiki w a Simba na kupewa nafasi ya Kutumbuiza siku ya Simba Day tangu msimu uliopita na msimu huu alifunika mbaya Kwa Mkapa.
Mbali na kutumbuiza Simba Day, Alikiba alishawahi kutumbuiza tamasha la Azam wakati huo akiwa Yanga na maisha yake yanaendelea akiwa kipenzi cha Wana Msimbazi.
Nyota wa Bongo Fleva anayetamba ndani na nje ya nchi, anatajwa kuwa ni shabiki wa Simba lialia, na alishawahi kutumbuiza tamasha la Simba Day akiweka rekodi ya kutua uwanjani kwa Helkopta, na aliwahi kukaririwa akisema maneno haya akiwa Msimbazi; “Sikuzote unajua siwaambiagi watu mimi ni timu gani, mimi ni Simba. Mimi siwezi kujiita Simba nikashabikia Chui. Mimi ni Simba na timu yangu ni Simba ndio maana leo nipo hapa.”
Lakini baadae maneno haya yalibadilikabaada ya kutangaza kujiunga na Yanga na kupewa nafasi ya kutumbuiza Yanga Day kutoa burudani, mbali na hilo alieleza sababu za yeye kujiunga an Yanga.
Diamond alielezea sababu ya kuhamia Yanga ni kuwa Haji Manara ndiye amemshawishi kujiunga na Yanga.
Mkali mwingine wa Bongo Fleva nchini, naye anatajwa kuwa ni Simba kindakindaki, lakini mwaja juzi msimu wa Yanga alikuja kuhamia Yanga na kupewa kutumbuiza Wiki ya Mwananchi iliyokuwa msimu wa pili tu na baada ya hapo amekuwa Mwananchi kamili akiendelea kuwapa raha Wana Jangwani.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, hapo awali alitambulika shabiki wa Simba, lakini alikuja kuhama na kuishabikia Yanga na anaendelea kuwa Mwananchi hadi leo.
Ni msanii wa Bongo Muvi, ambaye anajulikana ni shabiki wa Yanga kindakindaki , hivi karibuni amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana akiwa ametupia Jezi ya Simba ya msimu huu mpya.
wapo waliokuwa wanasema amepewa dili la kutangaza timu kwa kuwa yeye ni msanii.
Hata hivyo, mwenyewe amesisitiza ni kazi tu iliyompelaka kule, japo wanaomjua wanasema ndio kahama mazima na sasa anajiunga na chama la waliohama kambi.
Msanii wa Bongo Muvi, huyu alishawahi hama timu hizi mbili zaidi ya mara mbili, awali alikuwa timu ya Simba, akaja kutangaza kuhamia Yanga mwaka juzi, mwaka jana akatangaza kurudi Simba, kabla msimu haujaisha akatangaza amerudi Yanga.
Ni msanii wa kizazi kipya mwaka jana alitangaza kuhama Simba na kushabikia watani wao wa jadi, Yanga, na kutoa wimbo wa kuisifia timu hiyo na maisha yanaendelea hadi leo.
Hata hivyo, wanaomjua wanasema jamaa ni Simba lialia hadi alipohama kambi baada ya kushiriki matamasha kadhaa ya Msimbazi kwa kile alichodfai kwamba Simba ilikuwa ikisababishia msongo wa mawazo, kitu ambacho hakitaki.
Katika kile kinachoonekana kuwa ni penzi kukolea, mwanadada Paula mtoto wa msanii wa Filamu, Kajala Masanja na P Funk Majani, ameamua kuhamia Yanga kumfuata mzazi mwenzie, Marioo ambaye ni shabiki wa Yanga.
Awali, Paula naye alikuwa shabiki kindakindaki wa Simba, lakini kwa sasa amekuwa Mwananchi na kusema amemfuata baba mtoto wake.