Benki ya NMB leo Agosti 06, 2024 imezindua maboresho ya huduma kwa makandarasi ili kuimarisha sekta ya ujenzi nchini na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Miongoni mwa maboresho haya ni pamoja na Kukamilisha taratibu zote za kupata mkopo ndani ya siku 7 tu za kazi. Ongezeko la kiwango cha dhamana (Guarantee) za kuombea kazi (Bid Bond) mpaka Tsh Bilioni 5 bila kuweka dhamana.
Ongezeko la kiasi cha dhamana za miradi na malipo ya awali (Performance Guarantee na Advance Payment Guarantee) mpaka Tsh Bilioni 3 kwa mradi mmoja bila kuweka dhamana kwa taasisi zote za Serikali mfano TARURA, TANROADS, RUWASA na TANAPA nk.
Ongezeko la dhamana za miradi na malipo ya awali kwa kandarasi chini ya Halmashauri au Manispaa mpaka Tsh Bilioni 2 bila kuweka dhamana.
Hafla yetu imehudhuriwa na Mgeni Rasmi: Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Eng. Godfrey Kasekenya; Afisa Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi na viongozi mbali mbali wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),
Chama cha Makandarasi Tanzania (TUCASA) na Chama cha Wanawake Makandarasi Tanzania (TWCA) na wafanyakazi wa Benki ya NMB. Tunaamini kupitia masuluhisho haya, makandarasi wetu wataweza kuongeza ufanisi wao wa kazi na kushiriki katika miradi mingi zaidi.
#KonceptTvUpdates
FILBERT MPONZI ….Afisa mkuu wa wateja binafsi NMB BANK….Naibu Waziri wa Ujenzi MHANDISI GODFREY KASEKENYA. .